KITUO CHA KIJAMII CHA SIMBAS: 

Mwanzoni shirika hili lilianzishwa kama makao ya watoto yaliyo  jikita katika mpango endelevu wa kuwaunganisha watoto na familia zao, shirika letu limepitia mabadiliko na sasa  kituo wazi cha huduma za kijamii kituo kilifunguliwa rasmi mwezi Januari 2017. Kutuo chetu cha kijamii kimejikita na kuwezesha jamii inayotuzunguka na watoto kwa kuwapatia vifaa, elimu na msaada kwa watoto na familia. Tunaamini kwa kuwawezesha watoto, tumeiwezesha jamii yote kwa ujumla.

IMG_6546.JPG

SIMBAS CLUB

HUDUMA ZA KUTOKA

MPANGO WA EIK

SIMBAS CLUB:  Kupitia ratiba za baada ya masomo , Simbas club tunatoa programu mbalimbali za kielimu ambazo mara nyingi watoto hawazipati wakiwa mashuleni. Program hizi ni kama timu za michezo, darasa la muziki, maigizo, ngoma, sanaa na ubunifu pamoja na kujisomea na huduma maktaba ndani ya kituo.

MPANGO WA EIK:  Tunashirikiana na shule za kiserikali katika jamii yetu kwenye mradi wa kujifunza Kingereza na pia mradi wa Binti Yetu (Mpango mahususi kwa wasichana) katikaa masaa ya shule. Klabu yetu ya Kingereza inaendeshwa na walimu kutoka Simbas ikilenga kuboresha uwezo wa wanafunzi katika lugha ya Kingereza kwenye shule za msingi. Vilevile tunatoa mafunzo mahususi kwa Walimu katika mbinu bora za ufundishaji ili kuboresha na kuongeza ufanisi katika kufundisha kwa kuzingatia mtaala wa elimu Tanzania. Mradi wetu wa Binti Yetu unalenga katika kuwawezesha Wasichana na wanawake kwa kuwapa fursa kujifunza juu ya haki za wanawake, usawa wa kijinsia pamoja na elimu ya kijinsia.

HUDUMA ZA KUTOKA:  Kwa kufanya kazi na viongozi wa mtaaa, tunafanya miradi inayoendana na malengo ya shirika letu na mahitaji ya kijamii. Lengo letu ni kufanya kazi sambamba na serikali ya Tanzania katika kuboresha miundombinu iliyopo.