HISTORIA YETU:

Shirika la Simbas Footprints lilianzishwa Mwaka 2011 na Sybille Good kutoka Switzerland na Frida Marealle kutoka Sweden na limesajiliwa kama shirika lisilo la Kiserikali kwa namba (No. 07/NGO/08401) likifanya kazi maeneo ya Mji Mpya , Moshi Kilimanjaro.

Shirika  la Simbas mwanzoni lilifunguliwa kama kituo cha watoto, kwa kuwawezesha watoto tisa (9) walio yakimbia makazi yao kwa matatizo mbalimbali fursa ya kujiona wako katika familia tena na kujithamini. Watoto hawa walipatiwa huduma na kupewa malezi bora ikiwemo fursa ya kupata elimu. Kwa bahati nzuri, kufika mwaka 2014 watoto hawa walijenga mahusiano mazuri na ndugu/ wanafamilia mmoja au zaidi na hii ikapelekea kurejea katika jamii zao. Ni imani yetu kwamba kila mtoto anastahili kuishi katika jamii yake na kufurahia tamaduni zake, na kama shirika tunawawezesha na kuwahamasisha katika kujenga mahusiano mazuri na familia zao. Shirika la Simbas Footprints kwa sasa limejikita katika kuwawezesha wanafamilia kujikwamua ili kuchochea mazingira bora ya kuishi.

Tunaendelea kutoa msaada muhimu ili kuwezesha watoto hawa waliorejea kwenye familia zao kuweza kuishi vyema. Kwa sasa watoto wote tisa wameandikishwa shule ambapo shirika letu la Simbas lina fadhili.

 

 

DSC_3324.JPG